Croatia yaelekeza wahamiaji Slovenia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Croatia yaelekeza wahamiaji Slovenia

Croatia imeanza kuwaekeza maelfu ya wahamiaji kwenda kwa mpaka na Slovenia baada ya Hungary kufunga mpaka wake usiku wa manane siku ya ijumaa.

Serikali ya Hungary ilisema kuwa haijapewa njia nyingine mbadala, kufuatia kushindwa kwa muungano wa ulaya kulinda mipaka ya nje ya ulaya kutokana na kile ilichokitaka kuwa wahamiaji haramu.

Waziri wa mambo ya ndani wa Slovenia amesema kuwa wanatuma polisi zaidi kukabiliana na wahamiaji hao.