Uchaguzi Guinea:Alpha Conde aongoza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alpha Conde

Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Guinea yanaonyesha kuwa rais wa sasa Alpha Conde ameshinda kura za kutosha kuzuia kuwepo duru ya pili ya uchaguzi.

Huku asilimia 90 ya kura zikiwa zimehesabiwa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Conde yuko mbele ya mshindani wake mkuu Cellou Dalein Diallo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cellou Dalein Diallo.

Kiongozi huyo wa upinzani alisema wiki iliyopita kuwa alikuwa anajiondoa kwenye uchaguzi huo akidai kuwepo udanganyifu.

Uchaguzi huo ulifanyika licha ya janga la hivi majuzi la ugonjwa wa ebola ambalo liliwaua maelfu ya watu.