Uingereza yatakiwa kupokea wasyria 50,000

Haki miliki ya picha PA
Image caption Uingereza yatakiwa kupokea wasyria 50,000

Maaskofu wa kanisa la ki-Anglikana wanaiomba serikali ya Uingereza kuwapokea wakimbizi wengine zaidi ya elfu 30 kutoka Syria.

Maaskofu hao wanaitaka serikali ya waziri mkuu David Cameron kuwapa makao takriban wakimbizi elfu 50.

Cameron alikuwa ametangaza kuwa uingereza ingewapokea wakimbizi elfu 20 pekee katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu David Cameron akizungumza na wakimbizi kutoka Syria

Maaskofu hao walituma maombi hayo kwa serikali kwa njia ya barua ya kibinafsi kwa waziri mkuu mwezi uliopita.

Ujumbe huo wa barua hiyo sasa umewekwa wazi.

Barua hiyo inasema kuwa kiwango cha mateso ya binadamu kinachoshuhudiwa kwa sasa duniani, kinahitaji kushughulikiwa kwa haraka.

Askofu wa Durham, Paul Butler, anasema kuwa watu wengi wako radhi kuwasaidia wakimbizi wakiwasili Uingereza.

Haki miliki ya picha NC
Image caption Barua hiyo inasema kuwa kiwango cha mateso ya binadamu kinachoshuhudiwa kwa sasa duniani, kinahitaji kushughulikiwa kwa haraka

Askofu mkuu wa kanisa hilo jimbo la Aleppo nchini Ugiriki , Jean-Clément Jeanbart, ameiambia idhaa ya habari ya BBC kuwa licha ya kuwaelewa maaskofu hao ni vigumu kwake kukubali kuwa wanataka Uingereza iwapokee wakimbizi zaidi badala ya kuhimiza kurejeshwa kwa hali ya amani nchini Syria ilikupunguza mateso yanayowakumba .

Barua hiyo iliwekwa sahihi na maaskofu 84 kati ya 108 wa kanisa hilo duniani ambao waliahidi kuwashawishi waumini wao kuwapokea wakimbizi hao.