Kerry kukutana na viongozi Israeli na Palestina

Haki miliki ya picha EPA
Image caption John kerry kujadili ghasia zilizozuka upya baina ya WaIsraili na WaPalestina.

Waziri wa Mashauri ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, atakutana na waziri mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu juma hili, huko Ujerumani, kujadili ghasia zilizozuka baina ya WaIsraili na WaPalestina.

Bwana Kerry amesema atakutana pia na kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tangazo hilo limekuja wakati jeshi la Israil limewaondoa waumini kadha wa Kiyahudi

Tangazo hilo limekuja wakati jeshi la Israil limewaondoa waumini kadha wa Kiyahudi, ambao polisi wanasema, waliingia kinyume cha sheria, katika madhabahu ya kidini katika ufukwe wa Magharibi unaokaliwa na Israeli.

Kundi la WaIsraili 30, lilikwenda kwenye kaburi la Joseph, huko Nablus leo alfajiri, na kuzusha mapambano dhidi ya Wa-Palestina.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wimbi jipya la ghasia limesababisha vifo vya wa Israili 8, na zaidi ya WaPalestina 40

Kaburi hilo lilichomwa na Wa-Palestina siku ya Ijumaa.

Wa-Palestina wanne waliuwawa jana, wakishukiwa kuwa waliwashambulia ama walinuia kuwashambulia waIsraili kwa visu.

Wimbi jipya la ghasia limesababisha vifo vya wa Israili 8, na zaidi ya WaPalestina 40, katika majuma ya karibuni.