Kiongozi wa Japan aabiri manuari ya Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi wa Japan aabiri manuari ya Marekani

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, ametembelea manuari ya Marekani inayobeba ndege, na kuwa kiongozi wa kwanza wa Japani kufanya hivyo.

Alipanda USS Ronald Reagan, manuwari inayotumia nishati ya nuklia, kusini-magharibi ya Tokyo.

Wachambuzi wanasema hiyo ni ishara nyengine ya ushirikiano unaozidi, baina ya Japani na Marekani.

Hivi karibuni Japan ilibadilisha katiba yake iliyozuia nchi hiyo kushiriki kwenye vita; na hivo kuruhusu wanajeshi wa Japani kutumwa nchi za nje.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani na Japan pia zimeeleza wasiwasi wao, kuhusu mradi wa Uchina, kujenga visiwa katika maeneo yenye mzozo, ya bahari ya kusini ya Uchina

Marekani na Japan pia zimeeleza wasiwasi wao, kuhusu mradi wa Uchina, kujenga visiwa katika maeneo yenye mzozo, ya bahari ya Kusini ya Uchina.

Awali waziri mkuu huyo alishuhudia hafla ya maonyesho ya teknolojia ya majeshi ya wanamaji.

Ushirikiano mwema kati ya Japan na Marekani, unajiri huku Japan na China zikivutana kutokana na hatua ya China ya kuanzisha mradi wa ujenzi katika eneo linalozozaniwa la kaskazini mwa bahari ya China.