Mamia ya wahamiaji waingia Slovenia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji wakiingia Slovenia

Mamia ya wahamiaji wamevuka na kuingia Slovenia kutoka Croatia leo, baada ya Serikali ya Hungari kufunga mpaka wao. Wahamiaji 2,500 waliruhusiwa kuingia Slovena Jumamosi.

Serikali ya Slovenia imesema inaweza kuwashughulikia idadi kama hiyo tu kwa siku. Hungary ilisema kuwa ilifunga mpaka wake na Croatia usiku wa KUamkia Jum amosi kwa sababu viongozi wa Muungano wa Ulaya walishinda kukubaliana juu ya mpango wa kupunguza idadi ya watu wanaotafuta hifadhi.

Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch, alisema kuwa baridi imeongezeka na kutakuwa na changa moto nyingi zaidi.

Amesema kwa sasa ni msimu wa baridi umefika na idadi ya watu haijapungua. Kwa hivyo kuna watu wengi zaidi walio katika hali ya kusikitisha na wanaosafiri.

Msimu wa baridi utaongeza matatizo yao,kwa hivyo kile tunacho hitaji ni utaratibu tutakaotumia kuwasaidia kutoka mpaka mmoja hadi mwingine.

Bwana Babar Baloch alisema ameongeza kuwa itakuwa vigumu zaidi kwao, na kwa hivyo wanatarajia kuimarisha juhudi zao kama shirika la kuwashughulikia wakimbizi (UNHCR) na kuendelea kuhakikisha tunawasaidia wakati huu wote mgumu.