Papa Francis kuweka historia leo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Francis kuweka historia leo

Historia ya kanisa katoliki inatarajiwa kuandikishwa upya leo na Papa Francis huko Vatican.

Kivipi labda umejiuliza?

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis anatarajiwa kuwatawaza mume na mke kuwa watakatifu.

Louis na Zelie Martin walikuwa wapenzi waloishi katika karne 19.

Image caption Louis na Zelie Martin walikuwa wapenzi waloishi katika karne 19.

Wawili hao walifanikiwa kuwapata watoto 9, japo wanne waliaga dunia wakiwa bado wachanga.

Watano waliojaliwa kuishi hadi kuwa watu wazima waliishia kuwa watawa wote.

Mdogo zaidi kati yao ndiye aliyepata umaarufu zaidi na alifahamika kwa jina la Theresa kutoka Lisiex.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shughuli hii ya leo itafanyika katika ukumbi wa kanisa hilo huko Vatican ambapo mkutano wa viongozi wa kidini au makadinali unaendelea.

Theresa alisifiwa kwa maisha yake ya ukristo akitawazwa kuwa mtakatifu mwaka wa 1925.

Shughuli hii ya leo itafanyika katika ukumbi wa kanisa hilo huko Vatican ambapo mkutano wa viongozi wa kidini au makadinali unaendelea.