Slovenia yawapokea wakimbizi kutoka Croatia

Haki miliki ya picha v
Image caption Slovenia yawapokea wakimbizi waliotokea Croatia

Mamia ya wahamiaji wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchini Slovenia wakitokea Croatia, baada ya Hungary kuwanyima nafasi ya kuingia nchini humo ilipofunga mipaka yake usiku wa manane.

Serikali ya Slovenia imewahakikishia wahamiaji hao kuwa safari yao itaendelea vyema hadi wafike Austria, huku mipaka yao ikisalia wazi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hungary imefunga mipaka yake kwa wakimbizi

Slovenia imejenga kambi kadhaa za wakimbizi.

Waziri mkuu wa taifa hilo amesema kuwa wakimbizi walioko huko wanafaa kuhamishiwa kwingine ili kuwe na mpangilio muafaka na salama.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji 2500 waliingia nchini humo Jumamosi

Lakini serikali inasema kuwa inaweza tu kuwahudumia wahamiaji wapatao elfu 2,500 kwa siku.

Idadi kama hiyo ya wakimbizi ndiyo iliyowasili nchini Slovenia Jumamosi.