Maombi ya kunusuru uchumi Zambia

Image caption Maombi hayo yameitishwa kutokana na mfumuko wa bei ya vyakula na bidhaa nyingine muhimu mbali kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo

Viongozi wakuu katika serikali ya Zambia wanahudhuria siku kuu ya kitaifa ya kufunga na kuliombea taifa hilo ilikunusuru thamani ya sarafu yake.

Haki miliki ya picha thinstock
Image caption Sarafu hiyo imepoteza asilimia 45% ya thamani yake ikibadilishwa na dola ya Marekani.

Maombi hayo yameitishwa kutokana na mfumuko wa bei ya vyakula na bidhaa nyingine muhimu mbali kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo linalotegemea kwa kiwango kikubwa mauzo yatokanayo na madini ya shaba.

Kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa baa zote na vilabu vya burudani vimefungwa.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Edga Lungu anaongoza siku ya maombi ilikunusuru uchumi wa taifa hilo

Na si hayo tu waandalizi wa siku hii maalum ya maombi pia wamehakikisha kuwa hakuna uraibu wowote unaoendelea kwa leo hata mechi za kandanda ambayo hupendwa sana nchini humo zimeaahirishwa.

Thamani ya sarafu ya Zambia, Kwacha, imedorora mno na kupoteza takriban nusu ya thamani yake katika kipindi cha miezi 9 iliyopita.

Image caption Mechi za kandanda pia zimeahirishwa

Kufikia sasa Sarafu hiyo imepoteza asilimia 45% ya thamani yake ikibadilishwa na dola ya Marekani.

Hali hii watafiti wa maswala ya kiuchumi wanasema imetokana na mfumuko wa bei ya shaba ambayo imeanguka mno kufuatia mfumuko katika uchumi wa mteja wake mkuu China.

Rais Edgar Lungu anatarajiwa kuhutubia taifa hilo wakati wa hafla hiyo kubwa inayofanyika katika mji mkuu Lusaka.