Aliyehukumiwa kifo kwa kuzini Maldives aokolewa

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Mwanamke aliyehukumiwa kifo kwa kuzini Maldives aokolewa

Mahakama ya juu visiwani Maldives, imebatilisha hukumu ya kifo kwa kupigwa mawe mwanamke anayeshukiwa kupata mimba nje ya ndoa.

Mahakama kuu ilikuwa imemhukumu mwanamke huyo kufa kwa kupigwa mawe kwa kupatikana na hatia ya uzinifu chini ya sharia .

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama moja katika kisiwa maarufu kwa watalii na wanandoa cha Gemanafushi.

Mahakama ya juu hata hivyo imetoa hukumu mpya inayobatilisha uamuzi wa hapo jana ikisema kuwa sheria na kanuni za kimsingi zilikiukwa na mahakama ya chini.

Mabadiliko ya kikatiba nchini humo ilikuanisha sheria ya taifa hilo na sheria kali kwa misingi ya dini ya kiislamu 'Sharia'imeipa mahakama nchini humo uwezo mkubwa wa kutoa adhabu.

Adabu hi yo kupigwa kwa mawe hadi kufa ni hukumu ya kwanza japo mahakama imekuwa ikitoa adabu ya kuchapwa viboko hadharani.

Marufuku hiyo ya kutoshiriki zina hata hivyo haiathiri watalii na wanandoa wanaopenda kusafiri kisiwani humo kwa ajaili ya fungate.