Maelfu ya wakimbizi wakwama Slovenia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maelfu ya wakimbizi wakwama Slovenia

Maelfu ya wahamiaji wamekwama kwenye mpaka ya kuingia bara ulaya,baada ya mbinu mpya ya kuwadhibiti wahamiaji kutekelezwa.

Watu wengi, wakiwemo watoto wachanga wamekesha nje kwa baridi kali na mvua kwenye eneo lisilomilikiwa na mtu yeyote lililoko katikati mwa Croatia na Slovenia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wengi, wakiwemo watoto wachanga wamekesha nje kwa baridi kali na mvua

Kwa sasa wamepewa hifadhi ya muda karibu na kivukio cha mpakani baada ya shirika la msalaba mwekundu kuingilia kati.

Hali hii imesababishwa na hatua ya Slovenia ya kukataa kuwakubalia wakimbizi zaidi kuvuka mpaka wake na kuingia nchini humo.

Afisa mmoja kutoka chama tawala nchini Slovania, Tanja Fajon anasema juhudi za kutafuta suluhu zinaendelea.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kwa sasa wamepewa hifadhi ya muda karibu na kivukio cha mpakani

Mabasi yaliyojaa wakimbizi yaliegeshwa mbali na mpaka kusini mwa Serbia ambapo maelfu ya wakimbizi wamezuiliwa na polisi wa kulinda mpaka.

Inasemekana kuwa baadhi yao wamepigana na polisi wanaowazuilia wasiingia nchini humo.