Viongozi wa Ukawa waungana kumuaga Makaidi

Image caption Lowassa katika maziko

Aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa chama cha UKAWA nchini Tanzania, Dkt. Emmanuel Makaidi ambaye aliaga dunia siku tano zilizopita, alizikwa Jumanne mjini Dar es Salaam.

Image caption Mkewe Makaidi katika maziko ya mumewe

Marehemu Makaidi alikuwa pia mwenyekiti wa chama cha National League and Democrasy NLD, mojawapo ya vyama vilivyoungana kuanzisha chama kikuu cha upinzani, UKAWA, kinachoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa.

Upinzani ulisitisha kampeni kwa muda wa saa 24 kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

Image caption Ndugu na marafiki katika maziko ya Makaidi

Viongozi wa tabaka mbali mabli walihudhuria mazishi hiyo katika makaburi ya Sinza mjini Dar es Salaam.

Image caption Kaburi la Makaidi limewekwa maua

Makaidi alitarajiwa kugombea kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili.

Image caption Lowassa apewa usalama wa hali ya juu

Kufikia sasa wagombea sita waliotarajiwa kuwania viti vya ubunge katika uchaguzi huo wameaga dunia.