Bi Clinton kujibu maswali ya Congress

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwaniaji wa urais nchini Marekani bi Hillary Clinton anatarajiwa kutoa ushahidi wake mbele ya wabunge wa Congress leo

Mwaniaji wa urais nchini Marekani bi Hillary Clinton anatarajiwa kutoa ushahidi wake mbele ya wabunge wa Congress leo.

Kamati ya bunge inafanya uchunguzi kuhusu shambulio kwenye ubalozi wa Marekani mjini Benghazi nchini Libya lililofanyika miaka mitatu ilopita.

Balozi wa Marekani nchini Libya na watu wengine watatu waliuawa katika shambulio hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kamati ya bunge inafanya uchunguzi kuhusu shambulio kwenye ubalozi wa Marekani mjini Benghazi nchini Libya

Bi Clinton alikuwa waziri wa maswala ya kigeni.

Clinton sasa ni mpinzani mkuu kwenye kinyanganyiro cha tiketi ya urais kwa chama cha Demcratic.

Chama chake kimetaja uchunguzi huo kama mbinu ya chama cha republican ya kumchafulia jina.

Chama chake cha Democratic kinasema kuwa uchunguzi huu wa sasa ni njama ya wapinzani wao wa Republicans kumtupia udongo na kunyima nafasi ya kuwa rais.

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Chama chake cha Democratic kinasema kuwa uchunguzi huu wa sasa ni njama ya wapinzani wao wa Republicans kumtupia udongo

Tayari makamu wa rais Joe Biden amejiondoa katika kinyang'anyiro hicho.

Biden alikuwa anatarajiwa kuttoa ushindani mkali kwa bi Clinton.