Millen Magese
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke anayesaidia wanaotatizwa na endometriosis

Millen Magese ni shujaa Mwafrika aliyesahaulika. Na usidhani ni kwa sababu yeye alikuwa Miss Tanzania au kwa sababu yeye ni mwanamitindo tajiri na anayejulikana sana kimataifa na kutambulika na nembo kama vile Ralph Lauren.

BBC iligundua, Millen Magese ni shujaa aliyesahaulika kwa sababu amekataa kushindwa na ugonjwa hatari wa endometriosis, na amekuwa akihamasisha na kuhimiza wanawake wengine walioathirika na ugonjwa huu kutokufa moyo na kupambana nao.