Atembea kilomita 2000 kwenda kortini India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi mmoja wa dhehebu la jain ameamua kutembea kilomita 2000 kwenda kortini India

Kiongozi wa kidini ameitamausha mahakama moja nchini India alipoiambia kuwa hatoweza kufika mbele yake hadi baada ya miezi 8 kwani hawezi kuabiri gari..

Kisa ?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kwa mujibu wa kiongozi huyo magari ni moja ya raha za ulimwengu na ni haramu

Kiongozi huyo wa dhehebu la Jain alisema kuwa hawezi kupanda gari kwani ni inakiuka imani yake kali na kanuni za dini yake.

Bwana Acharya Kirti Yashurishwarji Maharaj anasema kuwa kwa sasa yuko katika jimbo la Kolkata,zaidi ya kilomita 2,000 kutoka mahakama hiyo iliyoko katika mji wa Ahmedabad Magharibi mwa India.

Image caption Maharaj anasema kuwa kwa sasa yuko katika jimbo la Kolkata,zaidi ya kilomita 2,000 kutoka mahakama hiyo

Yashurishwarji Maharaj anasema iliaupokee uongozi wake wa kidini ilimbidi kuukata ulimwengu na malimwengu kwa hivyo hawezi kushiriki mambo ya ulimwengu ikiwemo magari.

Mahakama hiyo hata hivyo imekatalia mbali ombi lake la kutaka kesi hiyo iahirishwe.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ushawishi wa watoto kujiunga na dini yeyote ni kinyume cha sheria

Bwana Acharya Kirti Yashurishwarji Maharaj anakabiliwa na tuhuma za kughushi vyeti rasmi vya serikali vilivyomruhusu kuwashawishi watoto wa kihindi kujiunga na itikadi hiyo ya Jain.

Ushawishi wa watoto kujiunga na madhehebu yeyote yanakwenda kinyume cha sheria za kuwalinda watoto nchini India.