Viongozi wa kanisa walipora sadaka Singapore

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Viongozi wa kanisa walipora sadaka Singapore

Mahakama nchini Singapore imewapata na hatia ya ufisadi, viongozi sita wa kanisa kongwe na kubwa zaidi nchini humo.

Muasisi wa kanisa la City Harvest, Kong Hee na watu wengine watano wanadaiwa kuwa waliiba dola milioni 17 hazina ya kanisa.

Yamkini Hee na washirika wake walikuwa wakizitumia pesa hizo kwa harakati zake zilizoshindwa za kumfanya mkewe kuwa nyota wa kimataifa wa nyimbo chapa Pop.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muasisi wa kanisa la City Harvest, Kong Hee na watu wengine watano wanadaiwa kuwa waliiba dola milioni 17

Dola zingine milioni 19 zilitumika kuficha kile walichofanya.

Viongozi hao wa kanisa hilo wanadai kuwa muziki ulikuwa njia mojawepo ya kuwafikia watu wasio wakristo, lakini mahakama ilikatalia mbali wazo hilo.

Sasa viongozi hao wamo katika hatari ya kufungwa jela maisha.