Waandamana wakiwa wamejihami Somaliland

Image caption Waandamanaji hao wanapinga hatua ya rais Ahmed Silanyo ya kukabidhi bohari ya kuhifadhi mafuta ya Berbera, mikononi mwa kikundi cha wafanyibiashara

Waandamanaji katika nchi iliyojitangaza kuwa huru ya jamhuri ya Somaliland wamefyatulia risasi malori ya kubeba mafuta kwenye barabara inayounganisha mji wa bandari wa Berbera na mji mkuu Hargeisa.

Gari moja lilipatwa na risasi.

Waandamanaji wengine waliojihami wameweka vizuizi kwenye barabara inayotoka Berbera.

Image caption Waandamana wakiwa wamejihami Somaliland

Waandamanaji hao wanapinga hatua ya rais Ahmed Silanyo ya kukabidhi bohari ya kuhifadhi mafuta ya Berbera, mikononi mwa kikundi cha wafanyibiashara wa kibinafsi.

Silanyo alipuuzilia mbali bunge la Somaliland ambalo lilikuwa limepinga mkataba huo likitaka bohari hiyo isalie kuwa rasilimali ya taifa.