Maandamano yaendelea Afrika Kusini

Image caption Maandamano yaendelea Afrika Kusini

Wanafunzi nchini Afrika Kusini wanaendelea na maandamano ya kupinga nyongeza ya karo ya vyuo vikuu.

Muungano wa wanafunzi nchini humo umeonya kuwa vyuo vyote vikuu nchini humo vitafungwa hii leo.

Image caption Muungano wa wanafunzi nchini humo umeonya kuwa vyuo vyote vikuu nchini humo vitafungwa hii leo.

Picha iloyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii inaonyesha wanafunzi wakikongamana nje ya chuo kikuu cha Pretoria wakiimba nyimbo za maandamano.

Awali mwenyekiti wa muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo (South African Students Congress) Luzuko Buku, aliiambia BBC kuwa makabiliano baina yao na polisi hiyo jana yaliwaongeza nguvu za kupigania haki zao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Jacob Zuma anatarajiwa kuwa na kikao na viongozi wa wanafunzi hapo kesho.

Rais Jacob Zuma anatarajiwa kuwa na kikao na viongozi wa wanafunzi hapo kesho.

Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imetangaza kuwa itaongeza karo kwa asilimia 10% hadi 12%.

Waziri wa elimu aliwaahidi wanafunzi kuwa nyongeza hiyo haitapita asilimia 6% mwakani 2016 lakini hata hilo wanafunzi wamekataa.

Image caption Wanafunzi wanataka waziri wa elimu atimuliwe

Maandamano haya yaliaoanzia shuo kikuu cha Johannesburg Witwatersrand sasa yameenea hadi chuo kikuu cha Cape Town, Rhodes , Stellenbosch , Fort Hare , chuo kikuu cha Free State na Cape Peninsula University of Technology.

Aidha ripoti zinaashiria kuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Pretoria nao wameanza kuandamana.