UN: Watu milioni 4 hawana chakula Sudan Kusini

Haki miliki ya picha
Image caption UN; Watu milioni 4 hawana chakula Sudan Kusini

Umoja wa mataifa UN, umeonya kuwa makumi ya maelfu ya watu huenda wakafa kwa njaa Sudan Kusini kutokana na mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe yanayozuia usambazaji wa vyakula vya msaada katika maeneo mengi ya taifa hilo changa zaidi duniani.

Image caption UN:Watu 30,000 katika jimbo la Unity hawajapata mgao wa vyakula vya msaada kufuatia mapigano makali

Umoja wa mataifa unasema kuwa watu 30,000 katika jimbo la Unity hawajapata mgao wa vyakula vya msaada kufuatia mapigano makali kati ya waasi na majeshi ya serikali ambayo yamezuia wahudumu wa mashirika ya misaada kuwafikia.

UN imesema kuwa Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya takriban miaka miwili yamewaacha takriban watu milioni 4 wakikabiliwa na baa la njaa.

Image caption UN imesema kuwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya takriban miaka miwili yamewaacha takriban watu milioni 4 wakikabiliwa na baa la njaa

Aidha shughuli za upanzi wa vyakula na pia mavuno zimesambaratishwa.

Kutokana na ukosefu wa amani wakulima wengi hawakuweza kupanda vyakula na hivyo kuna utashi mkubwa ambao umesababisha bei ya vyakula kuongezeka maradufu.

Haki miliki ya picha ap
Image caption UN sasa inataka pande zote husika ziwaruhusu wahudumu wake wafikishie vyakula na misaada wakaazi wa jimbo la Unity.

Baadhi ya familia zilizokimbia makaazi yao zimelazimika kula mlo mmoja wa samaki na maua ya maji kwa siku.

UN sasa inataka pande zote husika ziwaruhusu wahudumu wake wafikishie vyakula na misaada wakaazi wa jimbo la Unity.