Sweden yachunguza mauaji

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi ya Gothernburg,Sweden

Polisi wa Sweden wanaendelea kuchunguza ili kufahamu iwapo mwanamume aliyekuwa amefunika uso wake aliyewaua watu wawili, akiwemo mwanafunzi mmoja karibu na Gothenburg, alichochewa na mawazo ya ubaguzi wa rangi.

Mshambulizi huyo aliwaua watu wawili na kumjeruhi vibaya mwanafunzi kabla ya kupigwa risasi na kuawa na polisi.

Vyombo vya habari vya Sweden vilionyesha ripoti zilizosema kuwa mvulana huyo mwenye umri wa miaka 21 alipendelea kusoma habari za Wanazi na alionekana kuchukizwa sana na Uislamu na uhamiaji.