Majeshi ya Kenya yawaua Al Shaabab 15

Image caption Majeshi ya Kenya yawaua Al Shaabab 15

Jeshi la Kenya limewauwa wapiganaji 15 wa al shabaab katika makabiliano ya hivi punde zaidi.

Majeshi ya Kenya ambayo yako chini ya muungano wa Afrika AMISON, yalishambulia kambi ya Al shabaab Kusini mwa Somalia.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kenya kanali David Obonyo '' jeshi hilo la Kenya lilikabiliana na wapiganaji wa Al shabaab katika kambi ya wapiganaji hao ya Yantoi karibu na mto Juba na kuweza kuwauwa wapiganaji wa Alshabaab kumi na watano.''

''Makabiliano hayo yalitokea mwendo wa saa kumi na moja Alfajiri''

AMISON lilitekeleza shambulizi hilo chini ya operesheni mahsusi ya Juba Corridor ambalo lengo lake ni kuwatimua wapiganaji wa Al shabaab kutoka maeneo hayo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanamgambo wa al shabaab, wameishambulia Kenya mara kadhaa;wanapinga kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini humo.

Miezi miwili iliyopita, jeshi la muungano wa AMISON lidhibiti mji wa Baardhere uliyopo katika bonde la Juba .

Aidha wametwaa makao makuu ya kundi hilo la Al shabaab ya Dinsor Kusini mwa Somalia.

Tangu hatua ya majeshi ya Kenya yaingie Somalia kupigana na wanamgambo wa al shabaab , Kenya imeshabuliwa mara kadhaa na wapiganaji hao ambao wanapinga kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini humo.