Uchaguzi wa urais kurudiwa Argentina

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Daniel Scioli anaongoza baada ya raundi ya kwanza ila atalazimika kupambana na mpinzani wake tena

Tathmini ya hivi punde zaidi ya upigaji kura huko Argentina inaonesha kuwa mgombea kiti cha urais anayeungwa mkono na chama tawala Daniel Scioli, ameshinda idadi kubwa ya kura zilizopigwa hapo jana.

Hata hivyo atalazimika kupambana tena na kiongozi wa upinzani aliyekuwa wakati mmoja meya wa mji wa Buenos Aires, Mauricio Macri katika marudio ya uchaguzi tarehe 22 mwezi ujao.

Hata hivyo matokeo rasmi yatatangazwa katika kipindi cha saa chache zijazo.

Rais Cristina Fernandez de Kirchner ambaye ametawala kwa mihula miwili hakuruhusiwa kikatiba kushiriki katika uchaguzi huu.

Image caption Mgombea kiti cha urais Argentina,Daniel Scioli,ameshinda raundi ya kwanza ya uchaguzi ila atapambana na Mauricio Macri katika raundi ya pili tarehe 22 mwezi ujao

Bi Cristina amesema kuwa ameiwacha Argentina katika hali nzuri kuliko alivyoipata.

Hata hivyo watu wa Argentina walipiga kura kumchagua rais atakayeirudisha nchi pamoja.

Wagombea wote waliwaahidi kushughulikia uchumi wa Argentina ambao umezorota, na kupunguza gharama za ustawi wa jamii - sera inayopendwa na watu lakini inawagharimu kiwango kikubwa cha fedha.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Scioli atalazimika kupambana tena na kiongozi wa upinzani aliyekuwa wakati mmoja meya wa mji wa Buenos Aires, Mauricio Macri katika marudio ya uchaguzi tarehe 22 mwezi ujao.

Lakini wadadisi wanasema, wapigaji kura walihitaji kuamua tu, mabadiliko yawe makali ya kiasi gani.

Bwana Daniel Scioli, anayependeleawa na rais Kirchener aliwahi kufanikiwa katika mashindano ya mashua, na kupoteza mkono wake katika mashindano hayo.

Hii ndio mara ya kwanza kwa uchaguzi mkuu wa urais kurudiwa katika historia ya Argentina.