Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump:Dunia ingekuwa bora na Gaddaffi na Saddam

Muaniaji kiti cha urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema kuwa dunia ingekuwa mahala salama zaidi kama tu Saddam Hussein wa Iraq na Maummar Gaddafi wa Libya wangelikuwa hai.

Bwanyenye huyo mbishi aliyasema hayo katika mahojiano na CNN baada ya kukashifu sera za kidiplomasia za rais Barrack Obama.

Image caption Japo tunamlaumu Maummar Gaddafi unadhani angekuwa hai magaidi wangekuwa huko ? La

Trump alisema kuwa maafa yanayoendelea Mashariki ya Kati yalichangiwa asili mia mia moja na sera haribifu za rais Obama na bi Hillary Clinton.

''Japo tunamlaumu Maummar Gaddafi unadhani angekuwa hai magaidi wangekuwa huko? La.'

'Angalia kwa makini hakuna Libya.'

'Libya tuliyoijua sasa imesambaratika kabisa'.

'Saddam Hussein alikuwa mtawala wa kiimla na tulijua kuwa hangeliwaruhusu magaidi kunawiri huko Iraq.'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ''Kwa hakika hali ilivyo sasa ni mbaya zaidi kuliko tulivyodhania wakati huo ukiukaji wa haki za kibinadamu umekithiri mno.''Trump

Sasa Iraq ndio Havard ama chuo kikuu zaidi cha ugaidi duniani.

'Kama ni maswala ya ukiukaji wa haki za kibinadamu.'

'Kwa hakika hali ilivyo sasa ni mbaya zaidi kuliko tulivyodhania wakati huo.'

Bwenyenye huyo anayetarajiwa kutwaa tikiti ya kuwania urais ya chama hicho cha Republican amesema kuwa anapania kuimarisha hadhi ya Marekani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump alisema kuwa maafa yanayoendelea Mashariki ya Kati yalichangiwa asili mia mia moja na sera haribifu za rais Obama na bi Hillary Clinton.

Aidha amesema kipengee muhimu katika utawala wake utakuwa kuimarisha uwezo wa Marekani kijeshi.

Trump amemlaumu Obama kwa kugawanya taifa.

Amesema kuwa nia ya utawal wake itakuwa kuwaunganisha wamarekani wote bila kujali tabaka.