Ukosefu wa taa watatiza hesabu ya kura Pemba

Haki miliki ya picha
Image caption Shughuli ya kuhesabu kura kisiwani Pemba imetatizika mno kutokana na ukosefu wa umeme.

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imeripoti kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa ya juu mno.

Hiyo tume hiyo imesema ndio sababu watu wengi walisalia katika foleni hata baada ya kukamilika kwa muda wa kupiga kura kama ilivyotajwa katika katiba ya nchi.

Kulingana na sheria ya uchaguzi nchini humo,shughuli zote za upigaji kura hazipaswi kuendelea ifikiapo saa kumi jioni.

Kwa hivyo wale wapiga kura waliokuwa kwenye foleni muda huo ulipofika ndio walioruhusiwa kupiga kura hadi pale watakapomaliza.

Image caption Shughuli ya kuhesabu kura kisiwani Pemba imetatizika mno kutokana na ukosefu wa umeme.

Kwa sasa kwa mujibu wa mkurugenzi wa tume hiyo ya uchaguzi Kailima Kombo vituo vingi vya kupigia kura vimebadilika na kuwa vituo vya kuhesabu kura.

Mwandishi wetu Halima Nyanza aliyeko kisiwani Zanzibar amesema kuwa shughuli ya kuhesabu kura kisiwani Pemba imetatizika mno kutokana na ukosefu wa umeme.

''Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea kwa amani ila tu hakuna taa kwa hivyo wahudumu wa tume ya uchaguzi wanatumia mishumaa kuhesabu kura''

Image caption Shughuli ya kuhesabu kura kisiwani Pemba imetatizika mno kutokana na ukosefu wa umeme.

Anasema kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa kubwa katika vituo alivyovitembelea na kuwa shughuli yenyewe iliendelea kwa amani.

Mashindano yamekuwa makali kati ya wagombea wa chama tawala cha CCM, na umoja wa vyama vya upinzani.

Mgombea wa chama tawala, John Magufuli, alipambana na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye ali