Sumu yatumika kuua ndovu 60 Zimbabwe

Haki miliki ya picha b
Image caption Ndovu 60 wameuawa Zimbabwe kwa sumu ya Cynide

Mizoga ya ndovu zaidi ya 20 imepatikana katika mbuga kubwa ya wanyama nchini Zimbabwe.

Maafisa wa kulinda misitu na wanyama pori nchini humo wanaamini kuwa ndovu hao waliuawa kwa sumu aina ya Cynide.

Msemaji wao Caroline Washaya-Moyo amesema kuwa idadi hii ni kubwa mno hususan ikizingatiwa kuwa takriban ndovu wengine 40 walipatikana wameuawa kwa njia sawa na hiyo hivi majuzi tu.

Mwaka wa 2013 ndovu 300 walipatikana wameuawa kwa njia ya kutatanisha baada ya wawindaji haramu kupaka sumu kwenye chumvi .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwaka wa 2013 ndovu 300 walipatikana wameuawa kwa njia ya kutatanisha baada ya wawindaji haramu kupaka sumu kwenye chumvi .

Tukio hilo la kutamausha lilitokea katika mbuga ya wanyama ya Hwange.

Kufuatia mauaji ya ndovu hao wasiopungua 60 kuna hofu kuwa uwindaji haramu umerejea upya na kwa kishindo nchini humo.

uchunguzi unaendelea kubaini athari ya sumu hiyo kwa wanyama wengine kama waliathirika au la.