HRW:Wanafunzi wanasajiliwa jeshini DRC

Haki miliki ya picha
Image caption Wanafunzi wasajiliwa jeshini DRC

Wanaharakati wanaonya kuwa shule huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -DRC, zinatumika kuwaandikisha watoto ili kuingia jeshini.

Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani Human Rights Watch, linasema kuwa makundi yenye silaha yamekuwa yakiwateka wanafunzi wa katika majimbo ya Kivu ya kaskazini na kusini.

Katika ripoti yake, kundi hilo pia linayalaumu makundi ya waasi na jeshi la serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshi au kuhifadhia silaha.

Image caption Katika ripoti yake, kundi hilo pia linayalaumu makundi ya waasi na jeshi la serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshi

Human Rights Watch imeitaka serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ifanye jitihada zaidi ilikuwalinda watoto.

Mwaka wa 2013 Umoja wa mataifa uliwapatanisha serikali na makundi ya wapiganaji katika jitihada za kuleta amani na kukomesha uasi uliokuwa ukiendeshwa na kundi la M23.