Matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar

Wanawake Zanzibar Haki miliki ya picha Zanzibar Electoral Commission
Image caption Maafisa wa kituo cha kuhesabia kura shehia ya Saateni, Zanzibar wakihesabu kura.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imetoa matokeo ya uchaguzi wa rais ambayo yamehakikiwa kutoka baadhi ya maeneo visiwani humo. Kufikia sasa tume hiyo imetangaza matokeo kutoa majimbo 31 kati ya 54.

Matokeo hayo yaliyokuwa yametangazwa kufikia saa mbili jioni Oktoba 27 ni kama ifuatavyo:

Matokeo ya uchaguzi wa rais Zanzibar (Majimbo31/54)
Jina Chama Kura Asilimia
Khamis Iddi Lila ACT-W 189 0.1
Juma Ali Khatib ADA-TADEA 93 0.0
Hamad Rashid Mohamed ADC 252 0.1
Said Soud Said AFP 223 0.1
Ali Khatib Ali CCK 240 0.1
Ali Mohamed Shein CCM 139,557 57.9
Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA 257 0.1
Seif Sharif Hamad CUF 93,699 38.9
Taibu Mussa Juma DM 118 0.0
Abdalla Kombo Khamis DP 86 0.0
Kassim Bakar Aly JAHAZI 227 0.1
Seif Ali Iddi NRA 63 0.0
Issa Mohammed Zonga SAU 127 0.1
Hafidh Hassan Suleiman TLP 107 0.0

Zanzibar ina jumla ya wapiga kura 503,860 waliojiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Kwa habari zaidi kuhusu uchaguzi mkuu Tanzania bonyeza hapa uchaguzi: #tanzania2015