Mawaziri 5 waangushwa uchaguzini Tanzania

Makao makuu ya matokeo ya uchaguzi nchini Tanzania
Maelezo ya picha,

Makao makuu ya matokeo ya uchaguzi nchini Tanzania

Mwaziri watano wa serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi katika majimbo yao,huku wagombea wengine wa Ubunge maarufu nao wakiangushwa na Kamba ya upinzania katika matokeo ya kura yanayoendelea kutolewa kufuatia uchaguzi mkuu wa nchini humo uliofanyika Jumapili.

Mawaziri hao watano wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete inayomaliza muda wake ni Stephen Wassira Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk Steven Kebwe,Naibu Waziri wa Afya,Christopher Chiza Waziri wa Nchi,Ofisi ya

Rais,Uwekezaji na Uwezeshaji,Anne Kilango Malecela,Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Omar Nundu aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Mawaziri hao walioangushwa katika majimbo yao wanaungana na wabunge wengine maarufu katika Bunge la Kumi la Tanzania waliong'ara ambao kwa sasa wameshindwa kurejea.

Hata hivyo pia wamo mawaziri wa Zamani Cyril Chami na Omary Nundu.Tume ya taifa ya Tanzania inaendelea kutangaza matokeo ya Ubunge na Urais.