Teksi zasusia kumbeba msanii mweusi Australia

Image caption Taxi zasusia kumbeba msanii mweusi Australia

Msanii nguli raia wa Australia almaarufu ''Uncle'' amekiri kuwa amebaguliwa mara nyingi tu hata na madereva wa teksi wanaokataa kumbeba.

Jack Charles amesema kuwa katika siku tatu zilizopita madereva wa teksi wamesusia kumbeba mara 2 licha ya umaarufu wake kama 'Uncle'

Meneja wake Patrice Capogreco, sasa anasema kuwa msanii huyo anatafakari kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi madereva hao wa teksi na kampuni zilizowaajiri.

Tukio la kwanza lilitokea usiku wa Jumatano iliyopita mjini Melbourne msanii huyo Charles alipokuwa akitoka kwenye dhifa aliyotuzwa taji la ''Victorian Senior Australian of the Year''.

Image caption Msanii huyo anatafakari kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi

Yamkini alipomsimamisha dereva mmoja wa teksi alidai alipwe kwanza kwani ''alihofia msanii huyo hakuwa na pesa za kulipa''

Na hata kabla hajasahau tukio hilo la kibaguzi, 'uncle' kama anavyofahamika, alisimamisha teksi nyengine impeleke kwenye uwanja wa ndege wa Melbourne ijumaa.

'uncle' aliwachwa ameduwaa dereva mwengine wa taksi alipovurumisha gari lake na kutoweka.

Halmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari umeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.

Msemaji wake ameiambia BBC kuwa halmashauri hiyo haitavumilia ubaguzi wa aina yeyote.

Image caption Halmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari umeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.

Halmashauri hiyo ilionya kuwa ''madereva wa teksi sharti wawe tayari kumhudumia mgeni yeyote bila kumbagua kwa misingi ya rangi ,tabia ama jinsia''

''Nauli ya teksi kuanzia saa nne usiku sharti ilipwe na mteja kabla hajabebwa kuanzia saa nne hadi saa kumi na moja asubuhi.

''Uncle'' ameiambia BBC kuwa sio tukio la ajabu miongoni mwa wa-Australia wa asili.

Mara nyingi wa-Australia wa asili hulazimika kuomba msaada wa wageni kuwasimamishia teksi.