Rihanna akubali kuigiza katika filamu mpya

Rihanna Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rihanna ni mmoja wa wanamuziki wanaovuma sana duniani

Mwelekezi wa filamu kutoka Ufaransa Luc Besson amefichua kwamba mwanamuziki mashuhuri duniani Rihanna ataigiza kwenye filamu yake ijayo.

"Rihanna yumo ndani ya Valerian!!!!! ....na atakuwa mmoja wa wahusika wakuu!!" aliandika kwenye Instagram. "Nina furaha sana!!!😊"

Bado haijabainika Rihanna, ambaye jina lake kamili ni Robyn Rihanna Fenty, atakuwa akumuigiza nani.

Lakini ataigiza kwenye filamu hiyo pamoja na Dane DeHaan na mwanamitindo Mwingereza ambaye pia ni mwigizaji Cara Delevingne.

Filamu hiyo imetolewa kutoka kwenye tamthilia ya ajenti anayeweza kuishi katika majira tofauti anayeishi katika karne ya 28.

Filamu hiyo itazinduliwa Julai 2017.