UN kutaja mataifa yanayochafua mazingira

Haki miliki ya picha PA
Image caption UN kuchapisha majina ya mataifa yanyochafua mazingira

Inadaiwa kuwa joto limeongezeka kwa zaidi ya kipimo cha nyuzi joto mbili, na kuhatarisha zaidi sayari ya dunia.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya inayotarajiwa kutangazwa na Umoja wa Mataifa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Joto limeongezeka kwa zaidi ya kipimo cha nyuzi joto mbili, na kuhatarisha zaidi sayari ya dunia

Umoja huo unatarajia kuchapisha mpango mpya wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Mpango huo umewasilishwa na mataifa 146, yanapojiandaa kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.

Image caption Mpango huo umewasilishwa na mataifa 146, yanapojiandaa kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa

Ripoti hiyo inatazamiwa kuelezea kwa mapana na marefu zaidi hali ya sasa ya mazingira katika mataifa ambayo hayataweza kuzuia kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa sasa duniani.

Umoja huo vilevile unatarajiwa kuelezea waziwazi mataifa kadhaa tajiri au maskini ambayo yamesaidia kupunguza hewa chafu ya Carbon Dioxide.