Polisi 4 washtakiwa kwa kuua mshukiwa

Image caption Polis 4 washtakiwa kwa kuua mshukiwa

Maafisa wanne wa polisi wameshtakiwa baada ya kunaswa na kamera za siri (CCTV) wakimpiga risasi na kumuua mshukiwa mmoja wa uhalifu

Gazeti mmoja la Afrika Kusini, Sunday Times lilichapisha video hiyo iliyowaonesha maafisa hao wakimpiga risasi na kumuua mshukiwa wa uhalifu licha ya kuwa alikuwa amejisalimisha kwa polisi.

Afisa mwengine wa polisi anaonekana akimvurumishia mateke katika tuko hilo lililotokea katika barabara ya Krugersdorp city, Magharibi mwa Johannesburg

Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Times, polisi walikuwa wakimfukuza Khulekani Mpanza kwa tuhuma za kutekeleza wizi wa mabavu tarehe 19 Oktoba .

Polisi walionekana kuwa wamembana na punde wakumuua.

Maafisa hao walijisalimisha wenyewe kwa mikono ya sheria baada ya nyuso zao kuonekana katika video hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi walimuua dereva mmoja wa teksi kinyama kwa kumfungia nyuma ya gari lao na wakaondoka huku akiburutwa barabarani hadi akafa.

Msemaji wa afisi ya kusimamia shughuli za Polisi IPD, Grace Langa, wanne hao watajibu mashtaka yanayowakabili baadaye leo.

Mbali na mauaji ya kinyama, wanne hao watashtakiwa kwa kuzuia haki isitendeke.

Picha hiyo inaonesha mshukiwa huyo akitupa Pistol yake kabla yake kunaswa na polisi na kuuawa.

Hili sio tukio la kwanza kuwakumba polisi nchini Afrika Kusini, Mwezi Agosti, maafisa wanane wa polisi walishtakiwa kwa kuua dereva wa teksi kinyama.

Walipigwa picha wakimfungia dereva mmoja wa teksi nyuma ya gari lao na wakaondoka huku akiburutwa barabarani hadi akafa.