Waasi Syria watumia mateka kama ngao

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Syria Bashar Al Assad

Taarifa kutoka nchini Syria zinaeleza kwamba ,waasi nchini humo wanatumia askari mateka wanajeshi na wengine wenye uhusiano na serikali kama ngao yao ili kujikinga na mashambulizi ya askari wa serikali vya rais Bashar al-Assad.

Mkanda wa video uliooneshwa katika mitandao ya kijamii inaonesha wanawake na wanaume waliofungwa katika vikinga vya chuma vilivyoweka nyuma ya malori na magari hayo kuendeshwa taratibu katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.

Mmoja ya mateka ni amesema ni mmoja wa maafisa wa jeshi ametaka kusitishwa kwa mashambulizi ya mabomu katika eneo hilo.

Inasemekana video hiyo imetoka katika eneo linalokaliwa na waasi katika vitongoji vya mji wa Damascus,mahali palipotokea mashambulizi ya roketi ambalo liliua watu sabini katika eneo la soko mwishoni mwa juma lililopita.