Sekta ya utalii itaongeza kipato Tanzania?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ndovu

Sekta ya utalii Tanzania 2014, iliweza kuongeza pato la taifa kwa asilimia 14, ambapo ni sawa na billioni 8,252.7 za kitanzania, na kukadiriwa kupanda kwa asilimia 1.3 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2015. Kwa upande mwingine sekta hii haijafanya vizuri zaidi ukilinganisha na mali asili za utalii zilizopo nchini humo.

Pia, kumekuwa na zaidi ya nafasi za kazi 1,337,000 kwa mwaka 2014, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda sekta hii imekuwa ikipatwa na vikwazo vingi vinavyoweza kushusha nafasi za kazi kwa asilimia .

Hata hivyo kwa mjibu wa ripoti ya World Travel & Tourism Sector,2015 inakadiriwa kuwa mpaka kufikia mwisho mwa mwaka 2015 ongezeko litakuwa asilimia mbili tu ukuaji ambao ni mdogo sana na kwamba mbinu mpya zinahitajika kukuza utalii.

Haki miliki ya picha Sandeep kumar gir forest
Image caption simba

Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa shirika la kimataifa la JovagoTanzania anafafanua kwamba, Sekta hii ni muhimu sana, lakini haijaleta matokeo mazuri sana katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na inakadiriwa kuwa na uwezo wa kushuka iwapo ujangili utaendelea kutazamwa bila wasiwasi,kushindwa kuthibiti rushwa , pamoja na kukosa uzalendo wa kutosha wa utalii wa ndani".

Guzzoni kutoka Jovago anasema kumekuwa na ongezeko la ushuru usiokuwa na mpangilio, hii pia husababisha wawekezaji wa kigeni na wandani kukwepa malipo ya kodi au kulipa kwa kutumia vishoka, hivyo mchango halali wa kodi huishia kwa watu binafsi na si serikali"

Haki miliki ya picha NPL
Image caption Twiga

Hata hivyo wawekezaji wengi hasa wa mahotelini wanatumia aina ya bidhaa na vyakula vinavyoagizwa kutoka nje,kama vile nchi za China, South Africa au India, hii inasababisha sekta kuwa nyuma kimaendeleo kwa kutothamini bidhaa za ndani na kushindwa kuingiza pato lataifa.

Kwa upande wake, Eva Hellinge, Mratibu wa jukwaa la sekta ya utalii litakayofanyika mwishoni mwaka 2015, alifafanua kwamba utafiti unakadiria mchango wa pato la taifa kupitia sekta ya utalii unaweza kuongezeka kwa asilimi sita tu ndani ya mwaka 2015-2025,iwapo tu serikali ijayo ya Tanzania itaweza kukabiliana na vikwazo ndani ya sekta hii kwa kupunguza utozaji wa ushuru usio na mpangilio kwa wawekezaji na kuthibiti watoza kodi wasio rasmi yaani vishoka ambapo kunawez akuwa na ongezeko la la zaidi ya asilimia 20.

Ili kuboresha sekta ya utalii nchini Tanzania elimu ya darasani na katika sekta hii ni muhimu, inatajwa kuwa mhimu ili kuwa na kizazi kitakacho linda hifadhi ya utalii wa taifa hilo.