Wanawake wa Afrika: Jinsi ya kuchangia mjadala

Haki miliki ya picha
Image caption Mjadala wa Global Questions utaandaliwa Nairobi

Wanawake barani Afrika wamepiga hatua gani tangu kongamano la Beijing miaka 20 iliyopita kuweka malengo ya kuimarisha maisha ya wanawake kote duniani ?

Umoja wa Afrika ulitangaza 2015 kuwa 'Mwaka wa Kuwawezesha Wanawake' lakini nini kimebadilika?

Ngendo Angela ataendesha mjadala wa Global Questions mjini Nairobi mwezi Novemba ambapo Waafrika wa kawaida watahusika moja kwa moja au kwa njia ya mtandao kuuliza jopo la wataalam jinsi wanawake wanaweza kushiriki kikamilifu kushawishi maamuzi na kubadili hali ya baadaye ya bara la Afrika.

Tuma maswali yako kwa globalquestions@bbc.co.uk kuhusu nini maana ya usawa kwa wanawake barani Afrika.

Unaweza pia kuchangia #BBCGlobalQuestions kupitia Whatsapp. Tuma swali lako kuhusu wanawake Afrika na masuala ya usawa kwa +447497371629.

Image caption BBC pia inawatambua wanawake waliosahaulika Afrika wanaotekeleza mchango muhimu katika jamii