Boko Haram yafichua kiwanda cha mabomu

Haki miliki ya picha Boko Haram
Image caption Picha hizo zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama (Government Technical College Bama (GTCB)

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram wamezindua kiwanda wanachotumia kuunda mabomu na silaha zingine kali Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Haki miliki ya picha Boko Haram
Image caption Picha hizo zilitumwa kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba iliyosajiliwa nchini Cameroon.

Kupitia kwa mtandao wa WhatsApp picha hizo zilitumwa kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba iliyosajiliwa nchini Cameroon.

Haki miliki ya picha Contributor
Image caption Wapiganaji hao wakipaka rangi silaha zao

Picha hizo zinaonesha watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi hilo wakiwa kwenye karakana fulani wakitengeneza silaha zenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa.

Picha hizo zinaaminika kuwa zilipigwa katika jimbo la Borno nchini Nigeria.

Haki miliki ya picha Boko Haram
Image caption Mhandisi wa Boko Haram akiunda silaha

Wachunguzi wanasema kuwa picha hizo zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama (Government Technical College Bama (GTCB).

Haijabainika iwapo mashine hizo za chuo hicho anuai zilinaswa na maafisa wa jeshi la Nigeria au la.

Haki miliki ya picha Boko Haram
Image caption Sehemu ya silaha zilizoundwa na Boko Haram

Hata hivyo Bama ni moja ya miji iliyokombolewa na jeshi la Nigeria.

Haki miliki ya picha Boko Haram
Image caption Sehemu ya kwanza ya mifereji ikikatwa kutengeneza silaha

Licha ya waasi hao kupigwa na kuondolewa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa Nigeria kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ambayo yamewaacha wa Nigeria wengi wakishangaa wanakotoa silaha hizo kali.

Haki miliki ya picha Boko Haram
Image caption Huu ndio ushahidi wa kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.

Huu ndio ushahidi wa kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.