Nkurunziza atoa onyo kwa wapinzani Burundi

Image caption Nkurunziza atoa onyo kwa wapinzani, Burundi

Huku Burundi akiendelea kukabiliwa na ghasia kutoka wa upinzani baada ya kuchaguliwa kuhudumu madarakani kwa mhula wa tatu katika mazingira yenye utata, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametoa ilani ya mwisho kwa wale aliowataja kuwa watenda mabaya kujisalimisha.

Katika hotuba kwa taifa Nkurunziza amesema kuwa wale ambao hawatajisalimisha katika kipindi cha siku tano zijazo watashtakiwa kama maadui wa taifa.

Haya yanajiri wakati mauaji yakiendelea kuripotiwa katika mji mkuu wa Bujumbura.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nkurunziza, amewataka wapinzani kukomesha vurumai nchini humo.

Nkurunziza, amewataka wapinzani kukomesha vurumai nchini humo.

Anasema kuwa sheria mpya ya kukabiliana na ugaidi, itaanzishwa ifikiapo mwisho wa mwezi huu wa Novemba.

Watu kadhaa wameuwawa na milipuko imekuwa ikisikika kila kuchao, hasa mjini Bujumbura, tangu mwezi Aprili, pale rais alipotangaza azma ya kuwania muhula wa tatu.

Nkurunziza ametoa agizo wajiepusha na uhasama.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa kila siku nchini Burundi mwili wa mtu hupatikana ukiwa umetupwa mabarabarani

Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa kila siku nchini Burundi mwili wa mtu hupatikana kwenye mitaro kandokando ya barabara ukiwa umepigwa risasi ama kudugwa kisu kwenye kifua na kufungwa kwa kamba ishara ya mateso kabla ya mauaji.

Kwa hivi sasa picha na video zinazidi kuenea kwenye mitandao ya kijamii ya facebook.

Vyombo vya habari visivyo vya kiserikali vimefungwa huku shirika ya kupigania haki za kinadamu zikilazimika kuondoa wafanyikazi wao nchini humo kwa hofu ya kukabiliwa na vyombo vya dola.