Candy Crush imeuzwa kwa dola bilioni 5.9

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Candy Crush yanunuliwa kwa dola bilioni 5.9

Je unamiliki simu ya kisasa ?

Ikiwa jibu lako ni ndio, basi bila shaka umecheza mchezo wa kupanga pipi al Maaruf Candy Crush.

Mchezo huo umbao ni maarufu sana kwenye seimu na hata kwenye console na programu za michezo ya video sasa umekutanishwa na mchezo maarufu zaidi kwenye Console 'The Call of Duty'

kupitia kwa kampuni ya Activision Blizzard.

Activision ambayo inamiliki michezo ya Console ya World of Warcraft na Call of Duty, imesema kwa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa imeinunua kampuni ya King Digital Entertainment, inayomiliki mchezo wa Candy Crush.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ununuzi huo utagharimu dola bilioni 5.9

Ununuzi huo utagharimu dola bilioni 5.9

Ununuzi huo unaifanya Activision Blizzard kuwa ndio kampuni kubwa zaidi katika michezo ya kompyuta na simu za mkononi.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa michezo ya kielektroniki, ufuasi mkubwa unazidi kuegemea kwenye michezo ya kidigitali na hivyo ununuzi huu unatilia hoja hiyo pondo.