Polisi wavamia afisi za soka Ujerumani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wavamia afisi za soka Ujerumani

Polisi nchini Ujerumani, wamevamia makao makuu ya shirikisho la soka nchini humo, DFB, baada ya kushuku kuwa shirikisho hilo lilikwepa kulipa ushuru.

Kashfa hii inahusishwa na uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2006.

Maafisa kadhaa walichukua baadhi ya stakabadhi na vifaa kadhaa na tarakilishi.

Taarifa kutoka kwa muendesha mashtaka inasema kwamba, wanachunguza uhamishaji wa zaidi ya dola milioni saba kutoka kwa akaunti za shirikisho la soka nchini Ujerumani hadi kwa akaunti za FIFA.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption shirikisho la DFB limekanusha madai dhidi yake

Kumekuwa na madai kuwa fedha hizo zilitumwa ili kupata kura kwa niaba ya Ujerumani ili ipewe uwenyeji wa kuandaa kombe la Dunia- madai ambayo shirikisho hilo la - DFB linayakanusha.

Polisi pia wamevamia nyumba ya Rais wa sasa wa DFB na ya mtangulizi wake.