Rais wa Myanmar aonya dhidi ya kuchagua upinzani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Thein Sein amewaonya raia wa nchi hiyo dhidi ya kupigia kura chama cha upinzani cha Aung San Suu-Kyi.

Rais wa Myanmar Thein Sein amewaonya raia wa nchi hiyo dhidi ya kupigia kura chama cha upinzani cha Aung San Suu-Kyi.

Katika hotuba yake ya moja kwa moja ya redio, siku sita kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Thein, anasema kuwa shinikizo la mabadiliko ya haraka haraka litaitumbukiza taifa hilo katika lindi la mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Thein amesema kuwa Myanmar inayojulikana kama Burma huenda ikaingia katika matatizo yaliyozikumba mataifa ya kiarabu wakati maandamano yalilazimu serikali kadhaa kun'golewa madarakani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Chama cha Aung San Suu Kyi, kinatarajiwa kushinda viti vingi, lakini anazuiwa kikatiba kuwa rais wa nchi hiyo

Jenerali huyo wa zamani, ameelezea mabadiliko kutoka katika utawala wa miaka 50 wa kijeshi hadi utawala wa kiraia nchini humo.

Chama cha Aung San Suu Kyi, kinatarajiwa kushinda viti vingi, lakini anazuiwa kikatiba kuwa Rais wa nchi hiyo.

Wengi wana wasiwasi iwapo Suu Kyi anaweza kujenga uhusiano wa karibu na jeshi la Burma ambalo linaushawishi mkubwa.