Waangalizi wa uchaguzi TZ waipinga ZEC

Image caption Wanachama wa tume ya uchaguzi Zanzibar, ZEC

Waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu nchini Tanzania TEMCO wamesema kuwa wameshangazwa na hatua ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kudai kuwa uchaguzi visiwani humo haukuwa huru na wa haki.

Mwenyekiti wa TEMCO Dkt Benson Bana amesema kuwa amesema kuwa waangalizi wao waliokuwa katika vituo vitu mbalimbali visiwani humo waliridhishwa na uchaguzi huo.

Bw Bana pia amesema kuwa TEMCO ilishtushwa na tamko la Oktoba 26, 2015 lililokuwa lililokuwa limetolewa na viongozi wa CUF wakidai kushinda uchaguzi wa Zanzibar.

Mwenyekiti huyo ameisihi ZEC kufikiria upya umamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo.

Hata hivyo, amevishauri vyama vya siasa Zanzibar kuzingatia katiba na sheria.

Image caption Waangalizi wa uchaguzi mkuu nchi Tanzania

Akizungumzia uchaguzi wa Tanzania Bara, kiongozi huyo wa TEMCO amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu kwa Tanzania bara ulikuwa ni huru na wa haki na kwamba wapiga kura walijitokeza kwa wingi.

Hata hivyo kuna baadhi ya migogoro iliyosalia kutokana na uchaguzi mkuu, na waangalizi hao wamewataka wanasiasa kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

"Badala yake wanapaswa kuwa kiungo muhimu katika suala zima la kudumisha amani," amesema Bw Bana.