VW yakanusha dai dhidi ya Porsche na Audi

Haki miliki ya picha iStock
Image caption VW yakanusha dai la udanganyifu dhidi ya Porsche na Audi

Kampuni ya kuunda magari ya Volkswagen imekana madai kutoka kwa maafisa nchini Marekani kuwa baadhi ya magari yake ya kifahari kama ya Porsche na Audi pia yalikuwa yamewekwa programu ya kudanganya kuhusu utoaji hewa ya gesi chafu.

Shirika la kulinda mazingira nchini Marekani linasema kuwa takriban magari 10,000 yaliwekwa programu hiyo.

Volkswagen sasa inasema kuwa itafanya ushirikiano na shirika hilo la mazingira ili kutatua suala hilo.

Porsche ambacho ni kitengo cha Volkswagen inasema imeshangazwa na madai hayo ikisema ina uhakika kuwa magari yake yametimiza ubora utaohitajika.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Magari hayo aina ya Porsche na Audi ni sehemu ya Volkswagen.

Afisi ya kulinda mazingira ya Marekani imesema kuwa inashuku kuwa magari mengine 10,000 yenye uwezo mkubwa wa injini unaozidi 3,000 CC pia zinachafua mazingira .

Magari hayo aina ya Porsche na Audi ni sehemu ya Volkswagen.

Volkswagen imekiri kuweka mifumo ya kudanganya ndani ya magari milioni 11 zenye uwezo usiozidi 2,000 CC.