Uingereza: Mlipuko ndio chanzo ajali ya ndege

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mabaki ya ndege ya Urusi ililyoanguka Misri

Uingereza imesema huenda mlipuko ndio uliosababisha ndege ya shirika la ndege la Urusi kuangukia eneo la Sinai, nchini Misri na kuua abiria wote 224 waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Safari za ndege kati ya nchi za Misri na Uingereza na pwani ya mapumziko ya rasi ya Sharm el-Sheikh zimesitishwa kama tahadhari wakati maofisa kutoka nchini Uingereza wakiendelea kuangalia hali ya usalama katika uwanja wa ndege.

Hali kadhalika, safari za kutoka na kuingia katika rasi hiyo zimesitishwa na Ireland.

Mamlaka ya safari za anga nchini Urusi hivi karibuni walitoa tahadhari kuwa ni mapema mno kueleza nini chanzo cha ajali hiyo.

Mabaki ya ndege hiyo na kisanduku cheusi chenye kurekodi mwenendo wa ndege hiyo bado vinafanyiwa uchunguzi.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu, la Islamic State limerudia kukiri kuwa lilihusika na ajali hiyo.