Kikwete akutana na Maalim Seif wa Zanzibar

Image caption Kikwete afanya mazungumzo na Maalim Seif Hamad wa Zanzibar

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amefanya mazungumzo na makamu wa rais wa kwanza kisiwani Zanzibar ambaye ndiye mgombea Urais kupitia tiketi ya chama cha upinzani (CUF) Maalim Seif katika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna mkwamo wa kisiasa kisiwani humo baada ya Tume ya Uchaguzi(ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika .

Hatahivyo mwandishi wetu aliyezungumza na mkurugenzi wa maswala ya mawasiliano katika chama cha CUF amesema kuwa hakuna lolote la muhimu lililoafikiwa isipokuwa 'mazungumzo ya kawaida'.

Amesema kuwa wamehuzunika baada ya kubaini kuwa rais Jakaya Kikwete anakamilisha muhula wake wa uongozi hapo kesho.