Mwanaume auawa na minyoo yenye Saratani

Image caption Mwanaume auawa na minyoo yenye Saratani

Mwanaume mmoja ameaga dunia baada ya kuambukizwa saratani na minyoo madaktari wamesema.

Mhasariwa alikuwa ameambukizwa ukimwi na hivyo hakuwa na kinga dhidi ya tegu waliotega mayai ndani ya utumbo wake.

Tukio hilo liligunduliwa kufuatia ushirikiano kati ya wanasayansi nchini Uingereza na Marekani.

Ripoti hiyo ya kwanza ya aina yake duniani imechapishwa katika jarida la kitabibu la New England Journal of Medicine.

Madaktari kutoka Colombia walijaribu kungamua nini kilichokuwa kinamuuma bwana huyo, bila mafanikio tangu mwaka wa 2013.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 41 alidhaniwa kuwa anaugua vidonda vya kawaida vya tumboni lakini baada ya uchunguzi wa kina akapatikana kuwa na vidonda kwenye mapafu yake maini na katika viungo vyengine muhimu mwilini mwake.

Kwa wakati mmoja vidonda hivyo vilikuwa vyenye mduara wa sentimita 4.

Cha kustaajabisha ni kuwa seli zilizokuwa zikimea ndani ya utumbo wake zilikuwa ndogo kuliko kawaida.

Na baada ya kupigwa msasa ilibainika kuwa zilikuwa takriban 1/10 ya seli za binadamu.

Vipimo vya chembe hai viligundua kuwa zilikuwa ni mabaki ya tegu (tapeworm) iliyokuwa imemuambukizwa saratani.

Haki miliki ya picha thinkstock
Image caption Hili ni tukio la kwanza kwa binadamu kuambukizwa saratani ya aina hii

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza watafiti kubaini kuwa minyoo anaweza kumuambukiza binadamu saratani ya aina ya kipekee.

Daktari Atis Muehlenbachs, aliyegundua tukio hilo alijipata ameduwaa kwani ilikuwa ni maajabu.

''Haijawahi kutendeka kwa hivyo mimi nilikuwa najaribu tu ,,,siamini kwa hakika ,,siamini maanake uvimbe uliokuwa unanitatiza ni kama vile tegu walitega mayai yao ndani ya utumbo wa mwanamume huyu na baada ya muda mrefu yakaenea.''alisema dakta Muehlenbachs.

Kwa bahati mbaya aliaga dunia mjini Medellin Colombia siku tatau baada ya kugundua alikuwa ameambukizwa saratani na minyoo.

Duniani zaidi ya watu milioni 75 wanaminyoo aina ya tegu.

Hofu ya madaktari sasa ni kuwa huenda watu wengi zaidi duniani wanateseka kutokana na maambukizi yanayosababishwa na minyoo