Rais wa China aanza ziara Vietnam

Haki miliki ya picha Alexey Kudenko RIA Novosti Getty Images
Image caption Rais wa China aanza ziara Vietnam

Rais wa China Xi Jinping amewasili mjini Hanoi Vietnam.

Hiyo ndiyo ziara ya kwanza kwa rais wa China katika kipindi cha muongo mmoja.

Xi anaanza ziara ya siku mbili nchini Vietnam wakati kukiwa na msukosuko kuhusu eneo linalozozaniwa.

Rais Xi amepokewa kwa tahadhima kuu na mwenyeji wake.

Siku ya Ijumaa atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka taifa la kigeni kuhutubia bunge la Vietnam.

Haki miliki ya picha Kham Reuters
Image caption Maandamano ya kupinga sera za China yameshuhudiwa katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi

Lakini siku chache kabla ya ziara hiyo maandamano ya kupinga sera za China yameshuhudiwa katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa hatua za China za kudhibiti visiwa vinavyozozaniwa kusini wa bahari ya China zimezua ghadhabu kubwa nchini Vietnam huku China nayo ikiwa na wasiwasi kuhusu kuendelea kuboreshwa kwa uhusiano kati ya Vietnam na Marekani.