Facebook yapata faida kubwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Facebook yapata faida kubwa

Facebook imeandikisha faida kubwa ya dola $891m kati ya mwezi Julai na Septemba.

Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imeripoti ongezeko la asilimia 11% na na mapato ikilinganishwa na wakati sawa na hii mwaka uliopita.

Mwaka wa 2014 Facebook ilipata dola $806 ikilinganishwa na $891m ilizotia kibindoni mwaka huu kutokana na kukua kwa idadi ya watumizi wa mtandao huo wa kijamii.

Wawekezaji wamekuwa wakitafuta ishara kuwa Facebook imepata faida kutokana na mitandao yake ya Instagram na WhatsApp,ama hata dalili kuwa imeanza kuandikisha faida kutokana na ongezeko la idadi ya video zinazochapishwa kwenye mitandao hiyo.

Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa Facebook,Mark Zuckerberg amesema kuwa kampuni hiyo inalenga kukuza mapato yake katika siku za usoni.

Faida hiyo imetokana na kukuwa kwa idadi ya watumizi milioni 60 katika robo ya tatu ya waka huu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sasa Facebook inazaidi ya watumizi bilioni 1.55 kote duniani

Sasa Facebook inazaidi ya watumizi bilioni 1.55.

Kukuwa kwa idadi hiyo kubwa kunamaanisha kuwa mapato yataokanayo na matangazo ya kibiashara pia yanakuwa.

Kufikia sasa inakisiwa kuwa watumizi zaidi ya bilioni moja u nusu hutumia dakika 1 kati ya 5 wakidurusu mitandao ya kijamii ya Facebook amd Instagram.

Katika mwezi wa Septemba idadi ya watu waliotembelea mtandao wa Facebook imeimarika kwa asilimia 27% na kutimia watu milioni 894.