MOJA KWA MOJA: KUAPISHWA KWA MAGUFULI

Bonyeza hapa kupata habari za karibuni zaidi

1.12pm:Sasa rais Magufuli akiandamana na mkewe wanaondoka katika uwanja wa Uhuru baada ya kuapishwa rasmi.

1.09pm:Amewataka viongozi wa upinzani kushirikiana na serikali yake akisisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba rais aliyechaguliwa ni John Pombe Magufuli

Image caption Magufuli

1.06pm:Magufulu aipongeza tume ya uchaguzi kwa kufanya uchaguzi ulio huru mbali na vyombo vya usalama vilivyoimarisha amani.Awashukuru wanahabari kwa kuwaelimisha raia wa Tanzania

1.05pm:'Sasa ni kazi tu' awataka viongozi wa upinzani kushirikiana kwa lengo la kuendeleza na kuwahudumia watanzania

1.04pm:''Nashukuru wagombea wanzangu kwa kutupa chanagmoto,tumejifunza mengi kutoka kwao''.

1.03pm:''Natambua kwamba nina jukumu kubwa la kuwafanyia kazi watanzania,lakini hatahivyo tumuweke mungu mbele ili kutekeleza ahadi hizo.

1.02pm:Magufuli:Nawashkuru watanzania kwa kunichagua kwa kura nyingi ili kuongoza taifa kwa miaka mitano ijayo.

1.01apm:Magufuli:Nawashukuru viongozi mbali,mbali waliowasili hapa ili kujumuika nami katika sherehe hii muhimu.

1.00pm:Namshkuru sana mwenyezi mungu aliyetujalia kuwepo hapa pamoja na viongozi wa dini.

12.58pm:Na sasa ni wakati wa rais John Pombe Magufuli kulihutubia taifa.

Image caption Viongozi watambulishwa kwa umati

12.06am:Marais na viongozi mbalimbali waliowasili katika hafla hiyo watambulishwa kwa wananchi waliojaa katika uwanja huo.

Image caption Magufuli

12.00am:Na sasa kamanda wa jeshi anaomba rukhsa ya kuondoka uwanjani.

Image caption John Pombe Magufuli

11.56am:Ndege za kijeshi zinapita juu ya uwanja wa Uhuru kutoa heshima kwa rais mpya wa taifa hilo John Pombe Magufuli.

11.27am:Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima

11.23am:Mizinga 21 ya kumkaribisha rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli yapigwa

11.22am:Jeshi laomba rukhsa kutoka kwa rais mpya wa Taifa la Tanzania John Pombe Magufuli

Image caption Jukwaa la kula kiapo

11.20am:Jakaya Mrisho Kikwete sasa awasalimia viongozi waliofika katika jukwaa la waheshimiwa wakiwemo marais mbalimbali.

Image caption Kikwete

11.18am:Sasa jeshi lamuaga aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa makamu wake Gharib Bilal

10.55am:Makamu wa rais wa Kwanza mwanamke nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan aapishwa

Image caption Rais John Pombe Magufuli

10.51am:Rais mpya wa Tanzania apewa mkuki na ngao ya ishara ya kuchukua madaraka.

10.48am:''Mimi John Pombe Magufuli naapa nitatenda kazi zangu za urais kwa mujibu wa sheria na mila na desturi za muungano wa Tanzania,ewe mwenyezi mungu nisaidie''

10.47am:Rais mteule John Pombe Magufuli aapisshwa .Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pia amewasili hapa.

Image caption Bendera

10.45am:Na sasa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Kikwete amekuwa raia wa kawaida baada ya bendera ya utawala wake kushushwa hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

10.40am:Wimbo wa Taifa la Tanzania wapigwa na baadaye bendera ya rais Kikwete itashushwa ili kuashiria mwisho wa uoingozi wake.

Image caption Rais Jakaya Kikwete

Mizinga 21 ya kutoa heshima za mwisho kwa rais Jakaya Kikwete yapigwa.

Image caption Kikwete akizunguka uwanja

10.21am:Gari la gwaride la kijeshi lililombeba rais Kikwete sasa lauzunguka uwanja huo huku wananchi waliojjaawa na furaha wakimsalimia kwa kumpungia mkono.

10.20am:Na sasa msafara wa Rais Jakaya Kikwete wawasili katika uwanja wa Uhuru .KIkwete baadaye anaonekana kuingia katika gari rasmi la gwaride katika uwanja wa uhuru na kuwapungia mkono maelfu ya wananchi waliojaa katika uwanja huo.

10.15am:Rais Mteule John Pombe Magufuli awasili katika sherehe hizo na kulakiwa na jaji mkuu Othman Chande.

Image caption Uwanja wa Uhuru

9.48am:Rais wa Rwanda Paul Kagame anawasili katika uwanja wa uhuru na kuketi bega kwa bega na waliokuwa marais wa taifa hilo Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

9.47am:Rais wa kisiwa cha Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein amewasili katika uwanja wa Uhuru na anaonekana hapa akisalimiana na rais mstaafu wa Tanzania Hassan Mwinyi.Kumbuka kiongozi huyo wa Zanzibar aliongezewa mda wa kuhudumu katika kisiwa hicho baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais katika kisiwa hicho.

9.43am:Rais mteule John Pombe Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano kuchaguliwa nchini Tanzania tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.

Image caption Raia waliowasili uwanjani

9.39am:Vilevile aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga ambaye ni rafiki mkubwa wa rais mteule John Pombe Magufuli,rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph kabila pamoja na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni baadhi ya viongozi waliowasiliili kuhudhuria sherehe hiyo ya kihistoria.

9.35am:Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa katika hafla hii ni pamoja na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye tayari ameondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi akiandamana na Mkewe bi. Margeret Kenyatta na anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa sherehe hizi wakati wowote kutoka sasa

9.30am:Gwaride la kijeshi tayari limejiandaa vilivyo ikiwemo wanajeshi waliovalia sare za rangi tofauti hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Image caption Mapambo

8:00 am Mataifa mbalimbali yamekuwa yakituma risala za pongezi kwa Tanzania na kwa Rais Mteule John Magufuli.

Wa kwanza kutuma risala za pongezi walikuwa ni:

Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mohammed Abdelaziz.

Katika salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Bw Kagame amesema: "Kufuatia kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”

Naye Rais Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Sisi tuna uhakika kuwa chini ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.”

7:10 am Viongozi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo Jacob Zuma kutoka Afrika Kusini, Robert Mugabe kutoka Zimbabwe na Filipe Nyusi wa Msumbiji. Mhubiri mashuhuri kutoka Tanzania TB Joshua pia atahudhuria sherehe hiyo.

7:00 am Watumbuizaji wanaotarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe walifika uwanjani mapema na ala zao.

6:45 am Uwanja umeanza kujaa watu. Wengi wa waliofika mapema wanafurahisha kujipiga, kupigana na kupigwa pichwa kuweka kama kumbukumbu za siku hii.

Image caption Baadhi ya waliofika wamevalia mavazi yenye rangi za chama tawala CCM

6:30 am Uwanja wa Uhuru umepambwa ukapambika

Image caption Uwanja wa Uhuru

6:30 am Waandishi wa BBC wamo katika uwanja huo kukuletea habari kadiri zinavyochipuka.

Image caption Mwandishi wa BBC Leonard Mubali

6:30 am Sherehe ya kumuapisha Bw Magufuli inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Image caption Usalama umeimarishwa katika uwanja huo

6:00 am. HABARI YA ASUBUHI?

Rais Mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli anaapishwa leo kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.

Bw Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania.