IAAF yamshtaki Lamine Diack na mwanawe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF Lamine Diack

Shirikisho kuu la riadhaa Duniani, IAAF, limewashtaki watu wanne kuhusiana na kashfa ya matumizi ya madawa ya kusisimua misuli, kukiwemo mwana wa aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo, Lamine Diack.

Papa Massata Diack amewahi kufanya kazi kama mshauri wa shirikisho hilo.

Mkuu huyo wa idara ya kukabiliana na vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kusisimua misuli katika riadha katika shirikisho hilo ameshtakiwa pia kwa kukiuka kanuni za shirikisho.

Wameshtakiwa kwa kuficha habari kumhusu mwanariadha Mrusi aliyekuwa ametumia madawa ya kusisimua misuli.

Kesi hizo zitasikilizwa mjini London, mwezi ujao.

Viongozi wa mashtaka nchini Ufaranza wanasema kuwa Lamine Diack alipokea rushwa inayozidi dola milioni moja miaka minne iliyopita ili kuficha habari kuwahusu wanariadha hao Warusi.