Makamu wa rais wa Maldives afutwa kazi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bw Adeeb anadaiwa kupanga jaribio la kumuua rais

Bunge nchini Maldives limepiga kura kumfuta kazi Makamu wa Rais Ahmed Adeeb, akiwa ndiye mwanasiasa wa pili kuondolewa kutoka wadhifa huo katika muda wa miezi sita.

Hoja ya kumuondoa afisini ilipitishwa upesi kupitia hali ya tahadhari iliyotangazwa Jumatano.

Bw Adeeb alishtakiwa uhaini mwezi jana kuhusiana na mlipuko uliotokea katika boti ya Rais Abdulla Yameen.

Amekanusha tuhuma hizo lakini bado hajasimamishwa kizimbani kujibu mashtaka hayo.

Haki miliki ya picha ap
Image caption Bw Yemeen hakujeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea kwenye boti

Bw Yameen hakujeruhiwa kwenye mlipuko huo alakini mkewe aliumia.

Maafisa wa uchunguzi wa jinai wa FBI kutoka Marekani walichunguza mlipuko huo na wakasema hawakupata ushahidi wowote kwamba ulisababishwa na bomu.

Hoja ya kumwachisha kazi Bw Adeeb iliungwa mkono na wabunge wote waliopiga kura kwenye kikao hicho cha bunge.

Chama cha kikuu cha upinzani Maldivian Democratic Party (MDP), kilisusia kura hiyo.

Kiongozi wa MDP Mohamed Nasheed alifungwa jela mwezi Machi.